Chai Tamu – mapenzi na maisha mazuri

Haya, Imekuwa ni Kawaida sasa kwa Al Kags kuchapisha vitabu pepe, kama “Quarterly Colour Series of Poetry”, ambazo in safu za kizungu.

Hii leo natoa mwito kwa waandishi wote wa Kiswahili hasa malenga wa Kiswahili. Al Kags ana panga kuchapisha kitabu pepe cha Kiswahili kiitwacho, Chai Tamu. Kitabu chenyewe kitawahadhiri washairi mbali mbali.

Chai Tamu ni kitabu cha kwanza katika Safu ya vinywaji vya pwani – kitafwatiwa na Maji ya Ukwaju na Kahawa chungu (au tungu).

Isimu au vuma ya Chai Tamu ni Mapenzi na Maisha Mazuri.

Kama wewe ni mshairi wa Kiswahili, au wamjua Msanii wa Kiswahili, basi usisite. Mjulishe mara moja ili awasiliane na mimi – au wewe mshairi, nijulishe kwamba upo.

Kiswahili Kitukuzwe.

4 Comments
 • maitha
  Posted at 14:06h, 30 October

  naona watoa wito kwa malenga waliojificha kwenye mapango waamke !

 • Al Kags
  Posted at 14:43h, 30 October

  haswaaa…. ebu nisaidieni kuwatoa…

 • ndesanjo
  Posted at 19:41h, 30 October

  Nami nitatangaza wito huu kwa malenga wengine. Habari njema sana hii. Titi la mama litamu…

 • kisiki
  Posted at 05:39h, 27 March

  Nauliza vitabu ambavyo wasema vitakuwa kwenye tovuti viko wapi ama shughuli hii umeifikisha wapi…akhsanta.

  kwaheri

%d bloggers like this: