eti nini?

Mwanadada fulani eti kaniuliza kama najua kuandika kiswahili, kisha akapata mshangao nilipomjibu kihakika. Mwenyewe anaishi Bongo, kwao haswa ni huko Tz lakini makubwa ni kwamba yeye hajui kuandika kiswahili vile.

Haidhuru. Jambo la muhimu ni kwamba amejiunga na sarakasi ya wanablogu – hata usiku wa manane – hii sasa ninazungumza nae kwenye hotmail – hii sijui live waya, sijui live nini… saa nane usiku. Janga kubwa hili.

Nenda mcheki Sahara Soul Food umpe karibu. Na ukimuona, mwambie “kwisha yeye. kaingia pangoni hajitoi”

10 Comments
 • saharasoulfood
  Posted at 01:29h, 30 October

  Wewe! Ninajua kuandika Kiswahili, ila hai-flow kama English! Halafu inanichukua forever kuandika a simple paragraph. Nimeshajaribu sana, lakini nimeona tu niwaachilie nyie wazee. Labda siku mpja nitafanikiwa.

 • alexcia
  Posted at 02:41h, 30 October

  Al Kags,
  Hats off to ya’ll reppin’ propa wey in swa. Me all i can do is curse!

 • akiey
  Posted at 02:53h, 30 October

  Heko kwako kujitoa mhanga na matumizi murwa ya lugha halisi ya taifa. Huenda utamtia moyo dada huyu ajihamasishe nae pia kujieleza vyema zaidi na kwa ufasaha unaostahili.

 • Shiroh
  Posted at 05:59h, 30 October

  Nice layout!

  Kiswahili and I are strange bedfellows.

 • Al Kags
  Posted at 06:00h, 30 October

  @Alexcia, it will be interesting to see you learn. You write black american fairly well – I think.

  @Akiey, wamuona mwanadada mwenyewe amejitokeza hapa ili kujitetea… tutamuhimiza bila shaka. Pengine una maarifa 🙂 ya kuwawezesha wengine kuzungumza?

  Nawatafuta wa shairi wa kiswahili kwa kitabu changu kijayo. waelezee wengine…

  Al Kags

 • saharasoulfood
  Posted at 12:31h, 30 October

  Mzee wa Pwani, umechapia kidogo! Naona lugha imekupiga chenga. NKN (Nacheka Kwa Nguvu). Hii inatakiwa kusema KIJAYO au KIJACHO, “… Nawatafuta wa shairi wa kiswahili kwa kitabu changu kijayo …”

 • alkags
  Posted at 15:39h, 30 October

  mwanadada usitie shaka. Kuteleza sio kwanguka. NKN, Mambo haya ni yale yale… ‘japokuwa naweza kujitia kwamba nimezungumza lafudhi nyngine tu… kujitetea sishindwi.

  tupendane tujengane, bibiye…

  Al Kags

 • alkags
  Posted at 15:41h, 30 October

  @ Akiey, mwanadada tumemleta nyumbani waona. Uzungu ameutupilia mbali. Vidapa amevitupa sasa anazungumza kama sisi.

  Kazi nzuri, mwafrika

 • mwangi
  Posted at 18:22h, 30 October

  kazi bora. tujikazeni kisabuni ndugu zangu, tuitetee lugha yetu. undelea na umahiri huu wa lugha …

 • Betty
  Posted at 19:36h, 09 September

  Waswahili hamjambo? Za kuamka… kushinda? Hongereni kwa jitihada zenu kuitukuza lugha hii tukufu ya Kiswahili. Nami nawaunga mkono.

%d bloggers like this: