Site icon Al Kags

Ziara yangu Uhuru Park

Baada ya kutumia baadhi ya masaa ya asubuhi yangu katika eneo la kupumzikia la Uhuru, yaani Uhuru park, imenijia akilini kwamba maneno ya wakongwe wa kale wa Kiswahili waliosema, “tembea uone mengi”, yalikuwa ni ya ukweli mtupu.

Hii leo niliamua kwamba kwa vile niko na wakati, ningeweza kutembea kutoka nyumbani kwangu hadi Mjini Nairobi nikizuru mji wenyewe. nilipofika hapo Uhuru park, niling’amua kwamba kuna madiliko makubwa kwenye eneo hilo.

Nyasi zote zilikwa zimekatwa sare na ndogo ili zikaonekana kama zulia za hali ya juu za kutoka huko Uturuki. Watu walikuwa ni wengi na walio tapakaa katika shughuli mbali mbali. Kulikuwa na watu waliojiandaza kwenye nyasi na kulala, wapenzi walikuwa wameketi kando ya kidimbwi kilicho katikati ya eneo hilo, wakinong’onezeana maneno matamu, na wahubiri walikuwa wakijitayarisha kwa ibada za mchana wanazozifanya humo.

Ikielekeana na mnara wa jomo kenyatta kwa nyuma ukivuka gurufu la uhuru yaani Uhuru highway kuna mnara fulani ambao jina lake sikilipata lakini ulioandikwa maneno matatu katika kila upande: peace, love, unity (amani, upendo, umoja). Imani yangu ni kwamba mnara huo ulijengwa na kuwekwa hapo na serikali mojawapo ya kanu katika miale ya themanini. Katika mnara huo kulikuwa na harusi iliyokua ikiendelea na nilipofika mahali hapo, ilikuwa ndio wachumba hao walikuwa waki pigwa picha.

Ama kwa kweli lau ungelifika humo eneoni la Uhuru miaka mitano iliopita, zoezo lako halinge kuwa kama langu hii leo. uchafu ulikuwa ni mwingi, wizi ulikua kawaida, na minara ilikuwa imedhoofika kupindukia.

Ikizidi jiji la Nairobi limetwikwa kivumi kibaya kwa miaka kadhaa iliyopita hasaa kwa sababu ya uchafu, hali duni ya bara bara na ukosefu wa usalama na ulinzi. Nilipokumbuka kwamba tumeufunga mkutano mkubwa wa jumuiya ya serikali za kimwetu (yaani local governments) ndio africities, nilijiuliza kama huo mkutano ndio ulio fanya tufanye juhudi hizo.

“La hasha.” Gerald Owino, ni mfanyi kazi wa mji anayejihusisha na mambo ya usafi katika eneo la Uhuru. “Tulianza kuwa serious na hii kazi mwaka elfu mbili na tatu september, wakati mji ulianza kutupatia vifaa tunavyo hitaji. At least tumeona wadosi (matajiri) wanataka Uhuru park iwe poa na sisi tukitumwa tunafanya iwe poa.”

Ukimsikiza Owino utafikiri kwamba yeye hana motisha ya kazi yake lakini ukimwona akikwonyesha miti aliyoipanda, majina yake na usafi aliyoutekeleza, basi bila shaka utapata kuiona furaha yake.

Sally Koskei (ambaye hana uhusiano na aliyekuwa katibu wa baraza la mawaziri) ni afisaa wa polisi anayelinda usalama wa wananchi ndani ya Eneo hilo la Uhuru. Yeye na mwenzake, Albert Kandiri ni askari doria na wao huzunguka katika kila pembe ya Uhuru park ilikuhakikisha usalama.

“siku hizi huku hakuna wahalifu.” walinielezea kwa ari, “tukokazini bila mzaha.”

Nilipata kuzumngumza na wananchi kadhaa kama Milka wambui ambaye huja uhuru park kilasiku kwa maombi. milka mekuwa akienda uhuru park kila siku kwa miaka minane sasa, kuomba nawenzake na anasema kwamba ameyaona mabadiliko makubwa kwa mda huo.

“Zamani hungeweza kutoa viatu au kuongea kwa simu hapa. Ilikua ni hatari na hata kama hivyo viatu havikuibwa, basi ungepata rough time (wakati mgumu) na miba na vijiwe vidogo vidogo. Siku hizo tulikaa chonjo kwasababu chokora pia walikuwa si kidogo”

je, wakati umefika wa sisi kama wakenya kutabasamu?

Kesho nitakwenda kwenye eneo lingine hapa mjini, eneo la Jevanjee niwaelezee nitapata vipi.

mawazo yenu tumeni.

Exit mobile version