Nimekua nikiwaza kwamba hii lugha yetu pengine imedidimia kiasi kwamba hakuna atakae ijibu blogi hii. Aghalabu ni kwamba kiswahili sanifu hakizungumzwi tena humu nchini na hata nadra zaidi huko ulaya.
Nivipi hivi sisi wana-nyayo tumekipuuza kiswahili kama ambae hatukukisoma? Katika kazi yangu nimeona biashara kadhaa ambazo nina maono kwamba ni biashara za kesho. Kunazo zile za kusukumiza kazi, yaani outsourcing. Ukiwatafuta warembo wakuzungumza kimombo kutokea puani wapo wengi humu nchini na bila shaka biashara yako ya kusukumiza itafana hasaa ikiwa ni ya simu kutoka marekani na uingereza.
kiswahili twakiweza tena au tumekitupa?
nakumbuka nikiwa mchanga kulikua na wimbo kwenye runinga, ulioanzisha kipindi fulani cha watoto wa shule za msingi. wimbo wenyewe ulikua “kiswahili kitukuzwe, kwani lugha ya taifa…”
je, tufutilie mbali lugha hii au tuijenge?
Asante.
Tuijenge! Tuijenge!
Tuijenge, bila shaka!
Katika siku zangu za uanafunzi nyumbani Kenya, niliipenda sana lugha yetu ya kiswahili, na ujuzi wangu katika usanifu wa lugha ulikuwa wa kupendeza kweli.
Nilipenda sana haswa uhodari wangu katika utunzi wangu wa mashairi nilipokuwa kwenye shule ya upili.
Lakini lo, nikang’oka nyumbani nikaja Marekani na kiswahili changu sanifu nikakiacha nyumbani.
Na baada ya miaka zaidi ya kumi humu ng’ambo, Kiswahili sikielewi tena kama nilivyokielewa hapo awali, ijapokuwa bado ni kitamu sana kwa masikio yangu, haswa ninapotembelea mji wa Mombasa wakati wa likizo zangu.
Jambo ambalo linadhuru harakati za kukihifadhi Kiswahili ni ukosefu wa utumizi maofisini na haswa na wakenya chipukizi. Vijana chipukizi siku hizi hawajivunii, au hawana fahari na, lugha ya Kiswahili. Wao hupendelea kutumia “Sheng.”
Al Kags, I’ve always liked reading your essays. Glad you decided to come back!
Whispering inn, siamini kamwe kwamba kwako wewe, kiswahili kimetoweka. Ninavyokusoma, kiko ni kukikukuta tu kimazungumzo, pengine.
Wajua huku, Kiswahili chasemekana kuwa ni “uncool” kama hao chipukizi wanavosema. Ukikizungumza unaonekana kwamba wewe ni mtu wa ngazi za chini. lakini wakiona kwamba unakizungumza kwa dhati wao hufuata kama kondo.
Nilipata kwenda kotini juszi juzi nikampata hakimu mwenywe ana ng’ang’ana kuzungumza lugha kama ambae hakusoma. Niliona ajabu kwa mda mfupi tu, kisha nikakumbuka maswala ya ngazi.
Ah, wenzangu. Sisi tukipende.
Ms K, Nashukuru kwa maneno yako, japokuwa ni ya lugha nyingine. utaniona mara nyingi.
Al Kags
Tuijenge lugha yetu. Tuijenge!
Al Kagz, vipi mti!!? Lete mapya ya leo mazee,lol!
“Penye wengi hapaharibiki jambo” ni jambo la kuvutia mno kuwa Lugha sanifu inaendelea kupamba moto katika blogu. Pongezi tele kwako, kwa: Maitha, Ndesanjo na wabongo wote na pia kwa Marazzmatazz kwa kutilia bidii hatua hii.
Mimi na wenzangu kina Whispering Inn huenda ni wachanganya lugha lakini bidii ya kusanifisha lugha tusiwacheni kabisa.
Machizi hao wasemao Kiswahili ni lugha ya walio chini. Mataifa mengi yanakisoma Kiswahili na lugha inaendelea kukua. Shauri yao watabaki nyuma ili hali wazungum, waAsia na wengineo watakizungumza bila matatizo.
Ningependa kusema kwamba kiswahili kinafaa kitukukuzwa.Hivyo basi, ni jukumu letu kama wapenzi wa lugha tukufu ya kiswahili kuhakikisha kwamba kila wakati tunapowasiliana na wenzetu tufanye hivyo kwa kutumia lugha sanifu ili tusije tukawapotosha wengine walio na hamu ya kujua na kutumia lugha ya kiswahili kwa ufasaha wake.
Nilifurahi sana niliposoma blogi hii. Tangu nije masomo Marekani, sijapata fursa ya kuongea Kiswahili sanifu popote. Ni jambo la kusikitisha ukifika huku Merekani, watu wengi sana wanataka kujifunza kiswahili lakini hawapati nafasi ya kujifunza. Halafu watu waliobarikiwa sana kujua lugha hii, wanaitupa au wanaipa ‘cheo’ au hisia za chini. Ni lugha yetu. Ni kitu muhimu sana inayotufanya sisi kuwa kile ambacho tuko na hiyo ni sisi kuishi Afrika Mashariki.
Kwa hao wote wanaondeleza blogi hii, nawapa pongezi sana. Najua maandiko yangu yana makosa mengi na hiyo ni kwa sababu sijawa nikitumia lugha ya kiswahili wakati wowote.
J. C.